Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:31

Wataalamu waelezea Afrika ilivyoachwa nyuma wakati wa COVID


Bilionea Mo Ibrahim ni mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi ya Mo Ibrahim akizungumzia ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo ya COVID-19
Bilionea Mo Ibrahim ni mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi ya Mo Ibrahim akizungumzia ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo ya COVID-19

Wataalamu wanatoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji katika miundombinu ya afya ili kusaidia ukusanyaji wa takwimu, utafiti wa maendeleo kuhusiana na janga la COVID-19 na athari zake kwa uchumi wa Afrika.

Katika mazungumzo ya hivi karibuni kwenye kipindi cha televisheni cha Straight Talk Afrika cha VOA kilichopewa mada COVID-19 barani Afrika, virusi, aina mpya ya virusi na chanjo. Wataalamu walisema kwamba matatizo ya afya duniani yalifichua miundombinu duni ya afya barani Afrika.

Bilionea Mo Ibrahim ambaye ni mwanzilishi na mwenyekiti wa taasisi hiyo iliyopewa jina lake yenye makao yake mjini London alizungumza kuhusu ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo katika kilele cha janga hilo.

Alisema ubaguzi wa chanjo haukusaidia hali ya janga barani Afrika. Hata hivyo alisema bado ana matumaini kabisa kwamba janga hili kwa njia ya kushangaza litatusaidia sote kusonga mbele. Ili kuendelea mbele tunahitaji kutengeneza chanjo zetu wenyewe, alisema. Hatupaswi kutegemea nia njema au tabia ya busara ya watu wengine.

XS
SM
MD
LG