Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:34

Burundi yaondolewa vikwazo na Umoja wa Ulaya


Evariste Ndayishimiye, rais wa Burundi
Evariste Ndayishimiye, rais wa Burundi

Umoja wa ulaya (EU) umesema unaondoa vikwazo vyake vya kifedha dhidi ya Burundi.

Jumuiya hiyo imeeleza kwamba mazingira mazuri ya kisiasa na maendeleo yanayofanywa na serikali ya Burundi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo haki za binadamu na kurejea kwa hiari kwa wakimbizi nchini humo, ndyo yaliyopelekea uamuzi huo.

EU pia imegusia changamoto ambazo bado zipo katika masuala ya haki za binadamu, utawala bora, maridhiano na utawala wa sheria.

Kuondolewa vikwazo na umoja wa ulaya kunafuatia uamuzi kama huo uliofanywa na Marekani mwaka jana.

Vikwazo viliwekwa mwaka 2016 baada ya uamuzi wa rais wa wakati huo Pierre Nkurunzinza kugombea muhula wa tatu wa uongozi ambao ulisababisha maandamano yaliyopelekea vifo mitaani.

Nkurunzinza alifariki mwaka 2020 wiki kadhaa baada ya kuchaguliwa Evariste Ndayishimiye, mrithi aliyempendekeza.

Rais ndayishimiye amekaribisha uamuzi wa umoja wa ulaya na kusema kuwa nchi hiyo iko tayari kushirikiana na washirika wote.

XS
SM
MD
LG