Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:32

Wafungwa 38 wafariki kwenye janga la moto gerezani Burundi

Makamu rais wa Burundi Prosper Bazombanza akizungumza katika mkutano wa Umoja wa mataifa.
Makamu rais wa Burundi Prosper Bazombanza akizungumza katika mkutano wa Umoja wa mataifa.

Mashahidi katika mji mkuu wa Kisiasa wa Burundi wanasema kwamba moto mkubwa umeteketeza gereza moja lililojaa watu wengi nchini Burundi kabla ya mapambazuko  siku ya Jumanne, huku kukiwa na hofu ya hasara kubwa kwani wafungwa wengi walikuwa bado wamelala wakati huo.

Wanasema moto huo ulizuka takriban saa 10 alfajiri na kuharibu maeneo kadhaa ya gereza hilo.

Mfungwa mmoja akizungumza na shirika la habari la AFP kwamba wafungwa waliungua kutokana na moto huo, huku walioshuhudia wakisema kuwa waliojeruhiwa walikuwa wakisafirishwa hadi hospitalini kwa gari za polisi na jeshi.

Wengi wa wafungwa hao ni wanaume lakini pia kuna eneo tofauti la wanawake.

Kundi kubwa la polisi na askari walikuwa wamezunguka eneo hilo na kuwazuia waandishi wa habari kukaribia au kupiga picha, mashahidi walisema.

Chanzo cha polisi kilisema huduma za dharura zilichelewa kufika eneo la tukio, na lori la zima moto lilifika masaa mawili baada ya kuanza kwa moto huo.

Serikali ya Burundi imetoa idadi ya wafungwa 38 waliofariki na wengine 69 waliojeruhiwa.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana rasmi, lakini serikali inasema huenda ni ajali ya umeme.

Idadi hiyo imetolewa na makamu rais Prosper Bazombanza ambaye ametembelea jela hiyo akiwa na maafisa wengine wa serikali .

Jela hiyo ya Gitega ina uwezo wa kupokea wafungwa 400, lakini ilikuwa inahifadhi zaidi ya wafungwa 1,500 ikiwemo wale waliohukumiwa kifungo cha maisha kwa shutuma za kupanga njama ya kumuondoa madarakani rais wa zamani hayati Pierre Nkurunziza.

XS
SM
MD
LG