Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 07:52

Belarus kuwasaidia wakimbizi walio kwenye mpaka na Poland


Watoto wahamiaji kwenye mpaka wa Belarus na Nov. 13, 2021
Watoto wahamiaji kwenye mpaka wa Belarus na Nov. 13, 2021

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko Jumatatu amesema nchi yake inafanya kazi kuwarejesha makwao wahamiaji ambao wamekusanyika kwenye mpaka wa nchi yake na Poland.

Hii inaonyesha ni hatua ya kubadili msimamo wake ili kupunguza mvutano kabla ya mkutano wa Umoja wa Ulaya ambao unatarajiwa kuiwekea Minsk vikwazo vipya.

Maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kwa miezi kadhaa kuvuka mpaka kutoka Belarus na kuingia ndani ya Poland, lakini mivutano iliongezeka wiki iliyopita wakati juhudi za kutaka kuvuka mpaka zilizimwa na walinzi wa mpaka wa Poland.Poland

Brussels inaishtumu Belarus kuhimiza wahamiaji na kuwapeleka ndani ya Umoja wa ulaya kama hatua ya ulipizaji kisasi kutokana na vikwazo dhidi yake.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa ulaya wanakutana leo kujadili juu ya vikwazo vipya dhidi ya Belarus kufuatia mzozo huo wa wahamiaji.

Lukashenko amesema kabla ya mkutano huo kwamba Belarus haitaki hali ya mpakani kuzorota na kugeuka kuwa mzozo na kwamba inafanya kazi kuwarudisha nyumbani maelfu ya wahamiaji, wengi wao wakiwa wanatokea mashariki ya kati.

Umati mkubwa wa wahamiaji ulikuwa umekusanyika leo Jumatatu kwenye mpaka uliofungwa kati ya Belarus na Poland.

XS
SM
MD
LG