Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Belarus, Anatol Glaz, amesema katika mahojiano ambayo yamewekwa kwenye tovuti ya wizara hiyo Agosti 11, kwamba Minsk pia imebatilisha idhini yake ya kuteuliwa kwa Julie Fisher kama balozi wa Marekani nchini Belarus.
“Kwa kuzingatia kwamba Belarus haina tena uaminifu kwa utawala wa sasa wa Marekani, tunasimamisha ushirikiano katika miradi yote mipya, misaada na mipango inayoratibiwa na serekali ya Marekani hadi uaminifu huo utakaporejea,” Glaz amesema, akiongeza kuwa Minsk itakua na haki ya kutangaza hatua za ziada katika siku zijazo.