Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 09, 2025 Local time: 08:09

Jumuiya ya Kimataifa yaeleza wasi wasi kutokana na mapinduzi ya Sudan


Wanajeshi wapiga doria mjini Khartoum baada ya kutangazwa mapinduzi
Wanajeshi wapiga doria mjini Khartoum baada ya kutangazwa mapinduzi

Viongozi wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa nchi za Kiarabu na Umoja wa Ulaya pamoja na wa mataifa mengine wametaka kuachiliwa kwa viongozi wa kisiasa wa Sudan na kulaani juhudi za jeshi kuipindua serikali. .

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fatah al-Burhan ametangaza Jumatatu kupitia televisheni ya taifa kwamba amelivunja baraza tawala la mpito pamoja na serikali ya waziri mkuu Abdullah Hamdok na jeshi kuchukua madaraka.

Jenerali Abdel Fatah al-Burhan akitangaza amri ya dharura nchini
Jenerali Abdel Fatah al-Burhan akitangaza amri ya dharura nchini

Akilihutubia taifa Jumatatu, Jenerali Abdel Fatah al-Burhan amesema kwamba wanachukua uwamuzi huu β€œili kurekebisha njia ya kukamilisha mapinduzi ambayo Wasudan wanataka.”

Kiongozi huyo alitangaza hatua 9 zinazochukuliwa miongoni mwa hizo ni pamoja na kutekelezwa kwa amri ya dharura kote nchini.

"Nne kuvunja baraza huru la mpito na kuwaondowa wajumbe wake. Tano kuivunja serikali. Sita kuwaondowa wakuu wa majimbo. Saba kuwaondowa makatibu wakuu. Nane kuteuwa wakurugenzi wakuu kuhakikisha kazi za serikali na hatimae tisa kusitisha kazi za kamati ya kuwezesha utawala kufanya kazi," amesema Jenerali al-Burhan.

Mara moja maelfu ya Wa-sudan walishuka barabarani na kulaani mapinduzi hayo na ripoti za vyombo vya habari zinaeleza kwamba watu watatu wameuliwa walipopambana na polisi na 80 kujeruhiwa.

Moshi mkubwa ulionekana pia ukitanda hewani katika sehemu moja ya mji mkuu huo.

Jumuiya ya Kimataifa yalaani Mapinduzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kwenye ujumbe wa tweeter ametoa wito kwa viongozi wa kijeshi kumuachilia huru waziri mkuu Abdallah Hamdok na maafisa wengine wa serkali.

Amesema, "ni lazima kuheshimu katiba inayolinda juhudi kubwa zilizopatikana mnamo kipindi cha mpito wa kisiasa."

Wito huo umetolewa pia na Umoja wa Afrika, Umoja wa Nchi za Kiarabu, Umoja wa Ulaya na viongozi wa nchi mbali mbali za dunia.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya nchi za Pembe mwa Afrika

Jeffrey Feltman ametoa ujumbe wa tweeter akisema "Marekani imeshtushwa na ripoti za jeshi kuchukua madaraka ya utawala wa mpito, ikiwa ni kinyume na matakwa ya wa Sudan ya kuwepo na demokrasia. Na meguezi hayo hayakubaliki."

Feltman alikutana mwishoni mwa wiki na viongozi wa kijeshi na kiraia mjini Khartoum na kuwaeleza kwamba Marekani inaunga mkono utaratibu wa mpito wa kidemokrasia kuelekea utawala wa kiraia.

Jeshi la Sudan lapindua serikali ya Mpito
please wait

No media source currently available

0:00 0:09:18 0:00

​
XS
SM
MD
LG