Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:26

Walimu watatu wauliwa Kenya katika shambulizi la al-Shabab


Watu watatu wauliwa katika shambulizi la al-Shabab Garissa Kenya
Watu watatu wauliwa katika shambulizi la al-Shabab Garissa Kenya

Kamishna wa jimbo la kaskazini mashariki ya Kenya Nicodemus Ndalana, anasema wanaanzisha vita kamili dhidi ya kundi la kisomali laal Shabab.

Watu watatu wauliwa katika shambulizi la al-Shabab Garissa Kenya
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:25 0:00

Nicodemus Ndalana alikua anazungumza baada ya wapiganaji wakundi la al-Shabab kushamnbulia tena shule ya msingi ya Kamuthe Kaunti ya Garissa, jumatatu usiku. Shambulio hilo limesababisha vifo vya walimu wa tatu na moja kutekwa nyara kulingana na polisi wa kaunti hiyo.

Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa la AFP kamishna Ndalana anasema,"Ikiwa jamaa hawa wanatanagaza vita, wacha wafahamu kwamba hata sisi tumetangaza vita dhidi yao, na tutawafuta kokote pale wanapojificha. Na nina kuhakikishia vita vimeanza leo tuna maafisa tayari na wamepata amri ya kuwamaliza". anasema Ndalana.

Polisi wa Kenya wanasema shambulio hilo linaonekana kua mfululizo wa mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo tangu mwanzo wa mwaka mpya.

Taarifa ya polisi inaeleza kwamba mtoto moja alijeruhiwa kwa risasi wakati wanamgambo waliposhambulia shule ya msinigi ya Kamuthe Kaunti ya Garissa.

Mmoja kati ya walonusurika Anne Gideo ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kwamba shambulio lilitokea baada ua usiku wa manane hii leo.

"Walifika karibu saa saba usiku na kuanzakufyetua risasi kuanzia nyuma ya nyumba. Halafu ninadhani ni kiongozi wao aliyesimama mbele ya nyumba. Wakabaki hapo wakifyetua risasi kila sehemu'" amesema Gideo

Gideo ameendelea kusema kwamba washambulizi hawakondoka mara moja.

"Ghafla walipokua hapo tulimsikia mmoja akizungumzakwa Kiswahili akisema hakikisha hakuna hata mtu mmoja anabaki kua hai. Halafu wakaja katika nyumba hii nyumba ya wanaume na kuwaua wote", amesema Gideo

Taarifa nyingine ya polisi inaeleza walimu walouliwa ni kutoka sehemu nyinginje zakenya na kuna mmoja aliyetekwa nyara. Washambuliaji walimuagia huru mmuguzi kwasababi alikua mwanamke.

Wanamgambo hao walitia moto kituo cha polisi kilichokua karibu na kuharibu mnara wa mawasiliano ya simu wakati wa shambulio hilo la alfajiri.

XS
SM
MD
LG