Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 14:24

Macron achaguliwa rais mpya wa Ufaransa


Wafuasi wa Macron wakisherehekea ushindi wake katika duru ya npili ya uchaguzi wa rais, mjini Paris
Wafuasi wa Macron wakisherehekea ushindi wake katika duru ya npili ya uchaguzi wa rais, mjini Paris

Saa moja baada ya kufungwa vituo vya kura Ufaransa makadirio ya awali yanaonyesha mgombea kiti mwenye msimamo wa wastani Emmanuel Macron atapata ushindi mkubwa na kua rais mpya wa taifa hilo.

Mpinzani wake wa mrengo wa kulia mwenye itikadi kali Marinne Le Pen hakusubiri matokeo ya awali au rasmi kutoa hotuba yake ya kukubali kushindwa, bali aliwahutubia wafuasi wake mjini paris saa moja tu baada ya kufungwa vituo vya kupiga kura.

Le Pen amesema wapiga kura wamemchagua mtu atakae endelea na siasa za aliyemtangulia Francois Hollande, lakini kutoa wito kwa wafaransa kuungana na chama chake kuleta mabadiliko ya kisiasa.

Makadirio ya awali yanampatia Macron ushindi wa asili mia 65 .9 huku Le Pen akipata asili mia 34.5.

Jukwa ambalo Macron anatazamiwa kuhutubia wafuasi wake baada ya kupata ushindi.
Jukwa ambalo Macron anatazamiwa kuhutubia wafuasi wake baada ya kupata ushindi.

Macron mwenye umri wa miaka 39 anakua rais kijana kabisa katika historia ya Ufaransa. Kiongozi kijana wa mwisho alikua Louis Napoleon Bonaparte alipoapishwa 1848 akiwa na umri wa miaka 40.

Wafuasi wa Macron wameanza kusherehekea katika pembe mbali mbali za Ufaransa na makoloni yake huku umati mkubwa wa wafuasi wake wakimsubiri katika jumba mashuhuri la makumbusho la Louvre mjini Ufaransa ambako amepanga kusherehekea ushindi wake.

waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wametuma ujumbe wa pongezi kwa Macron kutokana na ushindi wake.

XS
SM
MD
LG