Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:18

Abe : Jaribio la Kombora la Masafa ya Kati ‘halivumiliki kabisa’


Rais Trump na Waziri Mkuu Abe
Rais Trump na Waziri Mkuu Abe

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kitendo cha Korea Kaskazini kurusha kombora la masafa ya kati ambalo aina yake haijatambulika katika bahari ya Japan “hakivumiliki kabisa.”

Abe amezungumza Jumamosi usiku akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais Donald Trump, Florida, Marekani, katika mazungumzo na waandishi wa habari yalioitishwa haraka sana.

Mkutano huo umefanyika katika chumba cha ornate ndani ya Jumba la Mar-a-Lago linalomilikwa na rais huko ambako Abe ametembelea pamoja na Trump wakati wa wikiendi.

“North Korea lazima iheshimu maazimio yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,” kiongozi huyo wa Japan amesema.

“Wakati wa kilele cha mazungumzo niliyofanya na Rais Trump, amenihakikishia kwamba Marekani itashirikiana na Japan kwa asilimia 100, na kuonyesha dhamira yake na uamuzi wake juu ya hilo, ndio maana rais yuko hapa na mimi katika mkutano huu na waandishi wa habari."

Trump alisema kwa kifupi kabisa katika mkutano wa waandishi, “Nataka kila mtu afahamu na kujua kwamba Marekani iko pamoja na Japan, ni mshirika wetu muhimu, kwa asilimia 100.”

Jaribio la Korea Kaskazini linatafsiriwa kwa upana zaidi kama ni changamoto ya uongozi wa Trump.

Korea Kaskazini ilitupa kombora hilo katika bahari ya Japan.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Jumamosi jioni, “kurushwa kwa kombora la masafa ya kati kumeonekana kaskazini-magharibi ya mji wa Kusong,” ikisema iligunduliwa kombora hilo limeangukia katika bahari ya Japan na “halikuwa linahatarisha usalama wa Marekani.”

Pyongyang haikutoa tamko lolote kuhusu urushaji wa kombora hilo, lakini wataalamu wamesema kombora hilo linawezekana likawa aina ambayo inauwezo wa kufika Japan, lakini sio Marekani.

Korea ya Kaskazini ilifyatua miripuko ya majaribio ya nyuklia miwili isiyo ruhusiwa mwaka jana na kurusha takriban dazeni mbili za makombora katika juhudi yake ya kupanua programu yake ya silaha za nyuklia na makombora.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alitangaza, katika hotuba yake wakati wa siku ya kuadhimisha Mwaka Mpya, kwamba nchi yake “imefikia hatua za mwisho” katika programu ya kutengeneza kombora la masafa marefu ICBMs( linaloweza kufika popote ulimwenguni), lakini wataalamu wa kimagharibi hawaamini kwamba madai hayo ni kweli.

Wakati huo Trump alijibu kitendo cha majivuno cha Kim juu ya silaha ya ICBM kwa ujumbe wake wa Twitter akisema:”Hilo halitatokea!”

XS
SM
MD
LG