Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 06:22

Trump Asisitiza Ushirikiano Muhimu Uliopo Kati ya Marekani na Japan


Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe

Rais Donald Trump amesema Washington, DC Ijumaa urafiki kati ya Marekani na Japan ni “wa dhati” na kusisitiza kuwa ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi mbili ni kiini cha amani katika eneo la Mashariki ya bara la Asia.

“Tunadhamira ya kuhakikisha kuna usalama Japan na maeneo yote yaliyoko chini ya mamlaka ya uongozi huo na kuendeleza kuimarisha ushirikiano huu muhimu,” Trump amewaambia waandishi kwenye mkutano White House wakati akiwa na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe.

Abe amesema yeye na Trump wamefikia makubaliano juu ya muundo mpya wa mazungumzo ya kiuchumi na juu ya ushirikiano wa kibiashara wa Pacific (TPP), yakiwa ni kati ya mambo watakayo zungumzia.

Trump amesema kuwa mahusiano yoyote ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili ni lazima yawe “huru, yahaki na yakunufaisha” pande zote mbili.

Japan ilikuwa na wasiwasi na athari za uamuzi wa Trump kujitoa kutoka katika mkataba wa kibiashara wa TPP, pamoja na mkakati wake wa “Marekani Kwanza” katika bara la Asia.

Abe amesema yapo matumaini ya kuandaa mpango wa kichocheo cha uchumi ambao utaweza kutengeneza maelfu ya ajira Marekani kupitia uwekezaji binafsi na waumma katika miundombinu.

Viongozi hao wawili tayari walianza mazungumzo ya siku mbili White House Ijumaa asubuhi kikao kilichowapa fursa kuimarisha mkataba wa ulinzi uliokuwepo muda mrefu kati ya nchi hizi mbili na kuimarisha mafungamano yao ya kiuchumi.

Trump, Abe na wake zao walitarajiwa kusafiri kwenda Palm Beach, Florida Ijumaa mchana kwa ajili ya mapumziko ya wikiendi katika jumba la Mar-a-Lago linalomilikiwa na Trump

Mkutano huo wa siku mbili ndio muda mrefu zaidi ambao Trump ametumia kuwa na kiongozi wa kigeni tangu awe rais Januari 20. Pia ni mara ya pili kwa Trump kukutana ana kwa ana na mshirika muhimu baada ya kumpokea Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May huko Washington wiki mbili zilizopita.

XS
SM
MD
LG