Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 28, 2025 Local time: 16:29

Trump asaini amri za kiutendaji kuboresha jeshi, uhamiaji


Rais Donald Trump, kushoto akisikiliza wakati Makamu wa Rais Mike Pence, wapili kushoto akimwapisha Waziri wa Ulinzi James Mattis.
Rais Donald Trump, kushoto akisikiliza wakati Makamu wa Rais Mike Pence, wapili kushoto akimwapisha Waziri wa Ulinzi James Mattis.

Rais Donald Trump amezuru Wizara ya Ulinzi Pentagon kama amiri jeshi mkuu Ijumaa, na kusaini amri mbili za kiutendaji wakati wa ziara yake.

Wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Waziri wa Ulinzi James “Jim” Mattis, Trump alifafanua ujumbe wake wa kiutekelezaji kuwa ni “ fahari ya kuimarisha” shughuli za kijeshi, ikiwemo ununuzi zaidi wa ndege na meli mpya na “vifaa” kwa ajili ya Jeshi.

Uchunguzi wa Kina

Katika hatua yake ya pili, Trump alisaini amri za kiutendaji, kufuatia ahadi za kampeni alizotoa juu ya “uchunguzi wa kina” wa wale wanaotaka kuhamia Marekani. Amesema utaratibu mpya wa usaili utatengenezwa ili kuwazuia magaidi wenye misimamo mikali ya Kiislamu” wasiweze kuingia nchini.

“Tunataka tu kuwaruhusu kuja nchini wale ambao wataendelea kuisaidia nchi yetu na kuwapenda kwa dhati watu wetu,” Trump amesema.

Ameongeza kuwa Marekani haiwezi kusahau kitendo cha Septemba 11, 2001 wakati iliposhambuliwa na magaidi, na kushambulia pia Pentagon, tukio ambalo watu 184 walipoteza maisha.

Wanaopinga amri hizo za kiutendaji inajumuisha taasisi ijulikanayo kama "No One Left Behind," ambayo imekuwa ikisaidia kuwaleta wakalimani waliotumiwa wakati wa vita kuja kuishi Marekani.

Kikundi hicho kimetoa tamko siku ya Ijumaa kikisema amri za kiutendaji zita “funga milango” kwa wakalimani wa kigeni ambao walipigana bega kwa bega na majeshi ya Marekani na hivi sasa wanataka hifadhi ndani ya Marekani.

Mkakati wa Kuishinda IS

Wakati wanatembelea Pentagon, Trump, Makamu wa Rais Mike Pence na Mshauri wa Usalama wa Taifa Michael Flynn walikutana na makamanda wa juu wa jeshi, akiwemo waziri wa ulinzi na mnadhimu wa majeshi yote.

Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema rais amewataka viongozi hao katika mkutano Ijumaa kutoa mapendekezo mapya jinsi wanavyoweza kuishinda Islamic State, pamoja na mapendekezo ya kuweza kujenga uwezo wa utayari na kuwekeza katika jeshi.

Afisa wa Marekani aliiambia VOA kabla ya mkutano huo kwamba rais atakuwa anatafuta njia mbadala za kupambana na kundi la Islamic State zilizokuwa hazikubaliki wakati wa utawala uliopita.

Kwa hali hiyo, maafisa wa juu wa ulinzi wanatarajiwa kutafuta vipaumbele makini katika kukabiliana na Islamic State.

Kwa mfano, afisa mmoja wa wizara ya ulinzi ameiambia VOA Ijumaa kuwa uongozi wa Obama uliweka vipaumbele viwili katika kuiridhisha Uturuki ambayo ni mshirika wake na kuishinda Islamic State.

Wito wa Trump

Moja ya mapendekezo ya kuishinda Islamic State ambayo inaweza kutolewa kama mkakati kuitikia wito wa Trump ni kuwapa silaha au kujenga uwezo wa wapiganaji wa Kurdish wanaojulikana kama YPG.

Suala la Marekani kuwasaidia kundi hilo ni nyeti kwa sababu mshirika wa NATO Uturuki analitambua kundi hilo kuwa ni la kigaidi.

Hata hivyo, wapiganaji wa Kurdish ni wengi na wanauwezo wa kuiteka Raqqa na wameonyesha ujasiri huo walipokuwa wakipigana na Islamic State huko Magharibi ya Syria na Mashariki yake.

XS
SM
MD
LG