Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 10:25

Mawaziri wawili wa Trump waapishwa


Makamu rais, Mike Pence amwapisha John Kelly
Makamu rais, Mike Pence amwapisha John Kelly

Bunge la Marekani limepiga kura ikupitisha uteuzi wa jeneralimstaafu, James Mattis kuwa waziri mpya wa ulinzi na pia kuidhinisha mstaafu mwengine Jenerali John Kelly kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Mattis na Kelly, wote umri wao ni miaka 66, wamekuwa wa kwanza kupitishwa katika baraza la mawaziri la Rais Donald Trump na wameapishwa kuanza kazi mara moja.

Baraza la Seneti lilikutana kupiga kura mara baada ya sherehe za kuapishwa rais wakati maandamano ya kusheherekea kuingia katika madaraka Trump yalikuwa yameanza.

Mattis alituma ujumbe wa heri kwa majeshi yote ya Marekani dunia nzima, akipongeza kazi wanazofanya kwa kusema “wao ndio macho na walinzi wa taifa hili” akiahidi kufanya juhudi zake zote “kuhakikisha majeshi yetu yako tayari kupambana leo na siku za usoni.”

Makamu wa Rais Mike Pence akimuapisha James Mattis
Makamu wa Rais Mike Pence akimuapisha James Mattis

Bunge lilimpa Mattis kura 98-1. Jumla ya kura za Kelly zilikuwa 88-11. Seneta ambaye hakupiga kura ni Jeff Sessions wa Alabama, ambaye yeye mwenyewe anasubiri kuthibitishwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani.

Trump amesaini makaratasi ya kumruhusu Mattis na Kelly kuanza kazi zao mpya baada ya dakika chache kuingia katika ofisi ya rais ya Oval Ijumaa jioni na kuanza majukumu yake. Makamu rais, Mike Pence baadae aliwaapisha mawaziri hao.

XS
SM
MD
LG