Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 04:00

Bomani: Hali ya Zanzibar Inapaswa Kushughulikiwa


Tanzania Election

Mwanasheria wa zamani wa Tanzania, Jaji Mark Boman amesema kuwa hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar inatishia mustakabali wa eneo hilo.

Mwanasheria huyo mkongwe amependekezwa kuundwa kwa jopo maalumu la wataalamu kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mwingine iwapo kutaonekana kuwepo haja ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Ikumbukwe uchaguzi wa Zanzibar ulifutwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa madai ya kuwepo vitendo vya ukiukwaji kutoka kwa wapiga kura na maafisa wa tume.

Mgogoro huo wa kisiasa umeikumba Zanzibar baada ya vyama vya CCM na CUF vyenye wafuasi wengi kuwaweka wagombea wao ambao wamekuwa wakichuana sana katika chaguzi zilizopita za visiwani humo.

Mara baada ya kufutwa kwa uchaguzi huo wa Oktoba 25, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ilidai kuitisha marejeo ya uchaguzi baada ya siku 90 jambo ambalo limezua mjadala mkubwa kutoka kwa vyama vya siasa na wafuasi wao.

Sikiliza taarifa ya mwandishi wetu George Njogopa kuhusu taarifa hiyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG