Wapiga kura wa Msumbiji walipiga kura Jumatano katika uchaguzi wa kwanza wenye ushindani mkubwa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo 1992, na kufanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1994. Kuna wagombea watatu wanaopigania kiti cha rais.
Wamsumbiji wapiga kura katika uchaguzi mkuu wenye ushindani mkubwa
13
Daviz Simango, mgombea kiti cha rais wa chama kipya cha upinzani cha MDM akiwa mjini Massinga, katika jimbo la Inhambane wakati wa kampeni za uchaguzi.
14
Mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa mgombea kiti cha rais wa chama cha MDM Daviz Simango katika jimbo la Nyassa.
15
Kampeni za uchaguzi wa mgombea kiti wa chama tawala cha Frelimo, Filipe Nyusi katika jimbo la Zambezi
16
Kampeni za uchaguzi za chama cha upinzani cha Renamo huko Pemba Oktoba 2014.