Jumapili, Februari 14, 2016 Local time: 04:35

  Habari

  Marekani mwenyeji wa mkutano wa ukimwi

  Watu milioni 34 wanaishi na virusi vya HIV na ukimwi huku watu milioni 1.7 walikufa kutokana na ugonjwa huo

  Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia siku ya ukimwi duniani Disemba Mosi 2011 katika chuo kikuu cha George washington mjini Washington DC
  Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia siku ya ukimwi duniani Disemba Mosi 2011 katika chuo kikuu cha George washington mjini Washington DC

  Mkutano wa kimataifa wa ukimwi umefunguliwa Jumapili nchini Marekani kwa wito wa serikali duniani kutokupunguza bajeti katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

  Mtaalamu mmoja wa ukimwi kutoka san Fransisco, Dr.Diane Havlir amewaambia wajumbe kwenye mkutano huo mjini Washington Dc, kwamba dunia ina nafasi ya “kuanza kutokomeza  ukimwi”.
  Amesema itakuwa hali ya kipekee kama azma ya dunia  itashindwa   katika suala hili kutokana na  kukata fedha kuzuia fursa hiyo. Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 34 wanaishi na HIV na ukimwi na watu milioni 1.7 wamekufa kutokana na ugonjwa huo mwaka 2011.

  Mkutano wa mwaka huu, unaitwa  “Turning The Tide Together” unatarajiwa kuwavutia watu zaidi ya elfu 20. Wageni wa ngazi ya juu akiwemo Rais wa zamani wa Marekani, bill Clinton, mke wa rais wa zamani wa Marekani, laura Bush, muimbaji Elton John na mcheza filamu Whoopi Goldberg.

  Zaidi ya watu 1,000 waliandamana katika mitaa ya Washington jumapili kutaka kuwepo na mtizamo zaidi kwa HIV na ukimwi.

  You May Like

  Jaji Scalia wa Marekani afariki

  Kifo cha Jaji Scalia kinatoa nafasi kwa Rais Barack Obama kuteuwa jaji mwingine wa mahakama kuu kabla hajaondoka madarakani baada ya uchaguzi wa Novemba mwaka huu. Scalia alikuwa mmoja wa majaji wakonsevativu katika mahakama kuu ya Marekani Zaidi

  Museveni ashiriki mdahalo wa urais Uganda

  Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Museveni kuhudhuria mdahalo wa wagombea urais pamoja na wagombea wengine saba. Rais Museveni aligoma kuhudhuria mdahalo wa kwanza Jan 15 akisema mdahalo ni swala la wanafunzi Zaidi

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.