Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:00

Marekani mwenyeji wa mkutano wa ukimwi


Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia siku ya ukimwi duniani Disemba Mosi 2011 katika chuo kikuu cha George washington mjini Washington DC
Rais wa Marekani, Barack Obama akihutubia siku ya ukimwi duniani Disemba Mosi 2011 katika chuo kikuu cha George washington mjini Washington DC

Watu milioni 34 wanaishi na virusi vya HIV na ukimwi huku watu milioni 1.7 walikufa kutokana na ugonjwa huo

Mkutano wa kimataifa wa ukimwi umefunguliwa Jumapili nchini Marekani kwa wito wa serikali duniani kutokupunguza bajeti katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Mtaalamu mmoja wa ukimwi kutoka san Fransisco, Dr.Diane Havlir amewaambia wajumbe kwenye mkutano huo mjini Washington Dc, kwamba dunia ina nafasi ya “kuanza kutokomeza ukimwi”.
Amesema itakuwa hali ya kipekee kama azma ya dunia itashindwa katika suala hili kutokana na kukata fedha kuzuia fursa hiyo. Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 34 wanaishi na HIV na ukimwi na watu milioni 1.7 wamekufa kutokana na ugonjwa huo mwaka 2011.

Mkutano wa mwaka huu, unaitwa “Turning The Tide Together” unatarajiwa kuwavutia watu zaidi ya elfu 20. Wageni wa ngazi ya juu akiwemo Rais wa zamani wa Marekani, bill Clinton, mke wa rais wa zamani wa Marekani, laura Bush, muimbaji Elton John na mcheza filamu Whoopi Goldberg.

Zaidi ya watu 1,000 waliandamana katika mitaa ya Washington jumapili kutaka kuwepo na mtizamo zaidi kwa HIV na ukimwi.

XS
SM
MD
LG