Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 10:15

Waziri wa Ulinzi wa Marekani amaliza ziara yake Afrika


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza na waandishi wa habari huko Nairobi, Kenya Septemba 25, 2023. Picha na REUTERS/Monicah Mwangi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumza na waandishi wa habari huko Nairobi, Kenya Septemba 25, 2023. Picha na REUTERS/Monicah Mwangi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amerejea Marekani Alhamisi baada ya kukamilisha ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika kama mkuu wa Pentagon.

Austin alianza ziara yake nchini Djibouti, ambako kuna kituo kikuu cha jeshi la Marekani katika bara la Afrika. Alipokuwa huko alikutana na viongozi wa Djibouti na rais wa Somalia, ambaye vikosi vyake, Austin alisema, vimepata maendeleo zaidi dhidi ya kundi la kigaidi la al-Shabab katika kipindi cha mwaka jana kuliko miaka yote mitano iliyopita.

Austin kisha alikwenda Kenya, ambako aliitembelea kambi ya Manda Bay iliyoko jirani na mpaka wa Somalia ambako lilitokea shambulio la kigaidi mwaka 2020 ambalo liliua Wamarekani watatu.

"Ujumbe hapa ni wa hdahiri kuwa vita dhidi ya ugaidi bado ni ajenda ya juu ya serikali ya Marekani," alisema Vincent Kimosop, mchambuzi wa sera katika shirika la Sovereign Insight.

Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Kenya walitia saini mkataba wa usalama wa miaka mitano ili kusaidia kufanya kazi pamoja dhidi ya tishio la ugaidi kwa nchi hizo mbili.

Austin pia aliahidi dola milioni 100 kusaidia ulinzi wa Kenya, wakati Kenya inajiandaa kuongoza ujumbe wa kimataifa wa kulinda amani nchini Haiti ili kukabiliana na ghasia za magenge.

Austin alimalizia safari yake kwa kwenda pwani ya magharibi ya Afrika, na kuwa waziri wa ulinzi wa kwanza wa Marekani kufanya ziara Angola. Maafisa wa mataifa yote mawili wana matumaini kwamba Angola inaweza kuachana na Russia kama muuzaji wake wa silaha na kuchagua silaha zilizotengenezwa Marekani.

Forum

XS
SM
MD
LG