Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 13, 2024 Local time: 16:35

Washukiwa wanne wa shambulio la Moscow ni raia kutoka Tajikistan


Washukiwa wa shambulio la Moscow wakifikishwa mahakamani, Machi 24, 2024. Picha ya Reuters
Washukiwa wa shambulio la Moscow wakifikishwa mahakamani, Machi 24, 2024. Picha ya Reuters

Watu wanne walioshtakiwa kwa mauaji kwenye jumba la tamasha mjini Moscow wametambulishwa na mamlaka kama raia wa Tajikistan, baadhi ya maelfu ya watu wanaohamia Russia kila mwaka ni kutoka nchi hiyo maskini iliyokuwa mwanachama wa Umoja wa Kisovieti ili kutoroka maisha ya kubaguliwa.

Pamoja na umaskini uliokithiri, Tajikistan imekumbwa na mivutano ya kidini. Waislamu wenye msimamo mkali walikuwa moja ya vyama vikuu vinavyoipinga serikali katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya 1990, ambavyo viliiharibu nchi.

Wanamgambo waliodai kuhusika na shambulio la Moscow lililoua watu 139, ni tawi ka Kundi la Islamic State kutoka nchi jirani ya Afghanistan, wanaripotiwa kuajiriwa kwa wingi kutoka Tajikistan.

Washukiwa hao wanne ambao walifikishwa katika mahakama ya Moscow Jumapili kwa mashtaka ya ugaidi walionekana kupigwa au kujeruhiwa wakati wakiwa chini ya ulinzi.

Mmoja alikaalishwa kwenye gurudumu akiwa amevalia vazi la hospitali.

Forum

XS
SM
MD
LG