Watu 37 walifariki na zaidi ya dazeni hawajulikani waliko magharibi mwa Indonesia baada ya mvua kubwa kunyesha na volcano baridi kutiririka na kuharibu nyumba, barabara na misikiti, maafisa walisema Jumapili.
Ujerumani imemuita balozi wake nchini Russia kwa wiki moja ya mashauriano mjini Berlin kufuatia madai ya udukuzi kwa chama cha Chansela Olaf Scholz.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili amesema kwamba serikali yake imepiga kura kwa kauli moja kufunga ofisi za kituo cha matangazo cha Al-Jazeera kinachomilikiwa na Qatar.
Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Msemaji wa rais wa Russia Dmitry Peskov amesema leo kwamba mazungumzo ya amani ya Ukraine bila Moscow hayana maana.
Wabunge wa Umoja wa Ulaya Jumatano wameidhinisha sheria ya uhamiaji, kwa matumaini ya kumaliza miaka kadhaa ya migawanyiko juu ya jinsi ya kushughulikia kuingia kwa maelfu ya watu katika bara hilo bila ya idhini.
Jaji mmoja wa mahakama ya rufaa ya New York amepinga ombi la Rais wa zamani Donald Trump, la kuchelewesha kesi yake ya jinai ya Aprili 15, wakati akipambana kuondoa kesi hiyo kutoka mji wa Manhattan, huko New York.
Taifa la Nicaragua Jumatatu Limetoa wito kwa Mahakama ya Juu ya Umoja wa Mataifa kusitisha misaada wa kijeshi ya Ujerumani na misaada mingine kwa Israel.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema hatua zilizotangazwa na serikali ya Israel kuongeza mtiririko wa misaada huko Gaza zinakaribishwa.
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen amewasili Guangzhou leo Alhamisi kuanzia ziara ya ufuatiliaji huko China ikiwa ni chini yam waka mmoja.
Waandamanaji wanaoipinga serikali wanakusanyika nje ya Bunge la Israel mjini Jerusalem na kuandamana hadi kwenye makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, wakitaka uchaguzi wa mapema na makubaliano ya kutekwa nyara huku kukiwa na hasira juu ya jinsi vita vya Gaza vilivyoshughulikiwa.
Moto katika klabu ya starehe ya usiku mjini Istanbul, Uturuki wakati ikifanyiwa ukarabati Jumanne umeuwa watu wasiopungua 27, maafisa na taarifa mbalimbali zimesema.
Wamarekani wana wasiwasi zaidi kuhusu wahamiaji halali kuweza kufanya vitendo vya uhalifu nchini Marekani kuliko ilivyokuwa miaka michache nyuma.
Kimbunga cha tropiki ambacho kimepiga katika kisiwa cha Madagascar wiki hii kimeripotiwa kuuwa takriban watu 18 na kuwakosesha makazi maelfu wengine, ofisi ya dharura ya taifa hilo imesema Ijumaa.
Rais wa Russia Vladimir Putin amewaonya washirika wa Ukraine, mataifa ya Magharibi, dhidi ya kutoa msaada wa vituo vya anga katika nchi zao.
Msururu wa mashambulizi ya anga mashariki mwa Syria Jumanne yaliua zaidi ya watu 10, akiwemo mshauri wa jeshi la Iran na mfanyakazi wa shirika la afya duniani (WHO), maafisa na ripoti zimesema.
Serikali ya Sudan Kusini Jumanne ilisema shule zitafunguliwa tena wiki ijayo baada ya kufungwa kwa wiki mbili kutokana na joto kali nchini kote.
Watu wanne walioshtakiwa kwa mauaji kwenye jumba la tamasha mjini Moscow wametambulishwa na mamlaka kama raia wa Tajikistan, baadhi ya maelfu ya watu wanaohamia Russia kila mwaka ni kutoka nchi hiyo maskini iliyokuwa mwanachama wa Umoja wa Kisovieti ili kutoroka maisha ya kubaguliwa.
Mwanamke wa kwanza kugombea urais kwenye uchaguzi wa Jumapili wa Senegal, huenda asipate ushindi, lakini wanaharakati wanasema kwamba kuwepo kwake kunasaidia kampeni ya muda mrefu ya kufikia usawa wa kijinsia kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi.
Pandisha zaidi