Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 15, 2024 Local time: 17:37

Miili 20 ya wahamiaji yapatikana kwenye bahari nchini Senegal


Boti ya wahamiaji kutoka Afrika ikiwasili kwenye pwani ya kisiwa cha Canary Uhispania, Julai 13, 2023.
Boti ya wahamiaji kutoka Afrika ikiwasili kwenye pwani ya kisiwa cha Canary Uhispania, Julai 13, 2023.

Waokoaji waliopoa zaidi ya miili 20 kwenye bahari kaskazini mwa Senegal Jumatano baada ya boti iliyokuwa inasafirisha wahamiaji kuelekea Ulaya kuzama, gavana wa eneo hilo ameiambia AFP, huku hofu ikiongezeka kuhusu wahamiaji waliotoweka.

“Zaidi ya miili 20 ilipatikana, gavana wa mkoa wa Saint Louis Alioune Badara Samb alisema kwa njia ya simu, akiongeza kuwa zaidi ya watu 20 waliokolewa.

Badara Samb hakusema ni abiria wangapi waliokuwa ndani ya boti hiyo lakini manusura waliiambia AFP kwamba mamia ya watu walikuwa ndani ya boti hiyo.

Mamady Dianfo, manusura kutoka eneo la Casamance kusini mwa nchi, alisema kulikuwa takriban abiria 300 wakati boti hiyo ilipoondoka Senegal wiki iliyopita.

Manusura mwingine, Alpha Balde alizungumzia abiria 200.

Forum

XS
SM
MD
LG