Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:26

Mazungumzo yavunjika Libya


Mpiganaji wa upinzani akiinua mkono wa ushindi katika kituo cha ukaguzi kati ya Tarhouna na Bani Walid, Libya
Mpiganaji wa upinzani akiinua mkono wa ushindi katika kituo cha ukaguzi kati ya Tarhouna na Bani Walid, Libya

Wapiganaji wa serikali ya mpito wanaouzingira mji wa Bani Walid wanatayarisha shambulio baada ya mazungumo na wafuasi watiifu kwa Ghadafi kuvunjika.

Mpatanishi wa Baraza la Mpito la Taifa NTC, Abdullah Kanshil amesema kwamba mazungumzo yalivunjika Jumapili pale wazee wa kikabila watiifu kwa Moammar Gadhafi walipokata pendekezo la kupelekewa madawa katika mji wa Bani Walid kwa sharti kwamba wapiganaji wa utawala wa mpito wataingia mjini humo wakati huo huo.

Mji huo uliyo kilomita 170 kusini mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli unahitaji kwa dharura madakatari, madawa pamoja na maji na chakula.

Bani Walid ni mji wenye watu wengi wa kabila kuu la Libya la Warfalla, walomsaidia Bw Gadhafi kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 42. Na wengi wa wapiganaji wa serikali ya mpito wanaouzingira mji huo ni watu kutoka kabila hilo la Warfalla.

Na kaika tukio jingine serikali ya mpito mjini Tripoli ilitangaza mipango ya kuwaandikisha watu elfu tatu miongoni mwa wapiganaji wake katika jeshi la taifa la polisi, na kuwatafutia walobaki kazi nyingine. Maafisa wa NTC wanasema mpango huo utawahusisha pia wale walopigana upande wa Gadhafi.

XS
SM
MD
LG