Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:51

Jalil:Gadhafi bado tishio kwa Libya na Dunia


Mustafa Abdul Jalil, mkuu wa baraza la mpito la taifa nchini Libya
Mustafa Abdul Jalil, mkuu wa baraza la mpito la taifa nchini Libya

Kiongozi wa baraza la mpito Libya asema Gadhafi bado ni tishio Libya na dunia huku upinzani nchini humo ukikaribia kuingia mji wa Sirte

Majeshi ya waasi nchini Libya yanaukaribia mji wa Sirte, mahali alipozaliwa Moammar Gadhafi, huku wakiendelea kumtafuta kiongozi huyo baada ya kuchukua udhibiti wa mji mkuu wan chi hiyo.

Makamanda wa waasi huko Misrata wanasema majeshi ya upinzani yanasonga mbele kuelekea Sirte kutoka magharibi siku ya Jumatatu yaliingia ndani ya kilomita 30 katika mji wa pwani ambao upo kilomita 450 mashariki mwa Tripoli.

Msemaji wa waasi alisema Jumapili kwamba majeshi yanayoipinga serikali yataikamata Sirte kwa lazima kama mashauriano na viongozi wa kikabila ya kujisalimisha kwake yatashindikana.

Bwana Gadhafi hajaonekana tangu wapiganaji waasi waukamata mji wa Tripoli na mji wa Sirte unaoonekana kama ni eneo moja ambalo Gadhafi anaweza kujificha.

Mkuu wa baraza la mpito la taifa, Mustafa Jalil alisema Jumatatu kwamba bwana gadhafi bado ni tishio kwa Libya na dunia.

Jalil pia aliitaka NATO kuendelea kusaidia, ambapo imekuwa ikifanya mashambulizi ya anga dhidi ya majeshi yanayoiunga mkono Gadhafi tangu mwezi Machi kwa mujibu wa mamlaka ya Umoja wa Mataifa ya kuwalinda raia. Maoni yake yamekuja wakati maafisa wa ulinzi kutoka nchi zilizohusika kijeshi nchini Libya walipokutana huko Qatar.

Wakati huo huo, Ufaransa ilisema inapeleka timu huko Tripoli Jumatatu kufungua tena ubalozi wake baada ya kuufunga kwa miezi sita wakati waasi wakipigana kuidhibiti nchi.

Shirika la kimataifa kwa wahamiaji lilisema Jumatatu meli yake imewaondoa kiasi cha wahamiaji 850 Wa-Libya waliokwama na waliokoseshwa makazi kutoka Tripoli siku moja kabla.

XS
SM
MD
LG