Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 30, 2024 Local time: 16:18

Kamishna wa Umoja wa Mataifa afanya ziara DRC


Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binaadamu Volker Turk akiwa Geneva Decemba 11, 2023. Picha na REUTERS/Denis Balibouse
Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binaadamu Volker Turk akiwa Geneva Decemba 11, 2023. Picha na REUTERS/Denis Balibouse

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za binadamu, Volker Turk amezitembelea kambi za watu waliokoseshwa makazi kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika ziara yake ya siku tatu Voleker anatarajiwa kuwa na mikutano na watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya jumuiya ya kiraia pamoja na rais Felix Tshisekedi na wajumbe wa serikali.

Volker alitembelea maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi ya karibuni yakishutumiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa ADF linalojihusisha na Islamic state ambapo karibu raia 10 hadi 15 waliuwawa mwishoni mwa wiki katika wilaya ya Beni.

Kamishna huyo wa maswala ya haki za binadam wa Umoja wa Mataifa amesema “nimekutana na kundi la watu ambao wamekoseshwa makazi kutokana na ghasia mbaya, mauaji ya halaiki yalifanyika katika nyumba zao na wamekuwepo hapa kwa takriban miaka mitatu. Matarajio yao ni kurejea nyumbani.”

Forum

XS
SM
MD
LG