Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 21, 2024 Local time: 20:23

Baraza la Wawakilishi la Marekani laidhinisha kumfungulia mashtaka waziri wa usalama wa ndani


Picha hii inaonyesha idadi ya kura zlizopigwa katika Baraza la Wawakilishi kumfungulia mashtaka waziri wa usalama wa ndani Alejandro Markos, Februari 13, 2024.
Picha hii inaonyesha idadi ya kura zlizopigwa katika Baraza la Wawakilishi kumfungulia mashtaka waziri wa usalama wa ndani Alejandro Markos, Februari 13, 2024.

Baraza la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na Warepublican Jumanne lilipiga kura ya kumfungulia mashtaka waziri wa usalama, wakimshtumu kutunga sera mbovu ambazo zimesababisha wahamiaji haramu kuingia kwa wingi Marekani.

Kwa kura 214-213, Baraza hilo liliidhinisha vifungu viwili vya kufungua mashtaka kwa kumshtumu waziri wa usalama wa ndani Alejandro Mayorkas kushindwa kutekeleza sheria za Marekani kuhusu uhamiaji, hali ambayo Warepublican wanadai ilisababisha wimbi kubwa la wahamiaji kuvuka mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Lakini hakuna matumaini kwamba Baraza la Seneti, lenye Wademocrat wengi, likapiga kura ya kumfuta kazi waziri Mayorkas.

Mayorkas amesema mara kadhaa kwamba hana jukumu lolote katika mzozo wa wahamiaji kwenye mpaka, akilaumu badala yake mfumo mbovu wa sheria za uhamiaji ambao bunge limeshindwa kuurekebisha.

Forum

XS
SM
MD
LG