Watu saba waliuawa na wengine 17 kujeruhiwa wakati sehemu nzima ya jengo la ghorofa huko Russia iliporomoka baada ya kushambuliwa na kombora la enzi ya Sovieti lililorushwa na Ukraine na kutunguliwa na Russia, maafisa walisema.
Vifaru vya Israel vimeingia ndani upande wa mashariki katika mji wa Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema Jumapili, baada ya usiku wa mashambulizi makali ya anga na ardhini, na kuua watu 19 na kujeruhi wengine kadhaa, maafisa wa afya wamesema.
Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo la Brazil la Rio Grande do Sul imeongezeka hadi 136, kitengo cha ulinzi wa raia katika eneo hilo kilisema Jumamosi, kutoka idadi ya awali ya 126 , huku watu wengine 125 wakiwa hawajulikani walipo.
Kuvurugika kwa misafara ya meli za mizigo katika Bahari ya Sham kumeongezeka na inatarajiwa kupunguza uwezo wa sekta hiyo kati ya nchi za Mashariki ya Mbali na Ulaya kwa kiasi cha asilimia 15 -20 katika robo ya pili ya mwaka, kikundi cha usafirishaji cha Maersk kilisema Jumatatu.
Takriban wahamiaji 107 wakiwemo wanawake na watoto wameachiliwa kutoka kizuizini katika mji ulioko kusini mashariki mwa Libya, msemaji wa kikosi cha usalama alisema Jumatatu.
Shambulio la anga la Israel Jumapili liliua watu wanne wa familia moja katika nyumba kwenye kijiji cha mpakani kusini mwa Lebanon, vyanzo vya ulinzi na usalama wa raia vimesema.
Uturuki haitafanya tena biashara na Israel yenye thamani ya dola bilioni 7 kwa mwaka hadi litakapopatikana sitisho la mapigano la kudumu huko Gaza na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapaletina bila ya kizuizi, waziri wa biashara wa Uturuki amesema leo Ijumaa.
Wanajeshi wa Russia wameingia kambi ya jeshi la anga nchini Niger ambayo ilikuwa inatumiwa na wanajeshi wa Marekani, afisa mkuu wa jeshi la Marekani ameliambia shirika la habari la Reuters, hatua inayofuatia uamuzi wa utawala wa kijeshi wa Niger kuwafukuza wanajeshi wa Marekani.
Mahakama kuu nchini Ghana imefuta mashitaka kwa Rais Nana Akufo-Addo ya kushindwa kuchukua hatua za haraka kuhusiana na mswaada unaopinga Ushoga (LGBTQ) iliyopitishwa na Bunge mwezi Februari, ilitua hukumu hiyo Jumatatu.
Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways Jumatatu limesema litasitisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kinshasa, baada ya mamlaka ya kijeshi kushindwa kuwaachilia wafanyakazi wake inaowazuia licha ya amri ya mahakama.
Watu 42 wamefariki katika mafuriko katika eneo la Mai Mahiu katikati mwa Kenya baada ya bwawa kupasuka mapema Jumatatu, na idadi ya vifo inaweza kuongezeka, polisi wamesema.
Mahakama ya mapinduzi ya Iran imemhukumu kifo mwanamuziki maarufu wa Iran Toomaj Salehi kwa mashtaka yanayohusiana na maandamano ya 2022-2023, wakili wake ameliambia gazeti la Iran la Sharq Jumatano.
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Soussa Jumanne alisema nchi yake iliwajibika kwa uhalifu uliofanywa wakati wa enzi ya utumwa na ukoloni, na amesema kuna haja ya kulipa fidia.
Maandamano ya wanaounga mkono Wapalestina yameongezeka katika vyuo vikuu vya juu vya Marekani siku ya Jumatatu.
Maafisa wawili wa ngazi ya juu wa Uingereza Jumanne wameomba serikali ifikirie tena mpango wake wa kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, wakionya kuwa hatua hiyo huenda ikawa ni matokeo mabaya kwa haki za kibinadamu pamoja na usalama wa wakimbizi.
Qatar inafikiria tena jukumu lake kama mpatanishi kati ya Israel na Hamas, waziri mkuu amesema jana wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Doha akiwa na mwenzake wa uturuki.
Kombora la Russia Jumatano liliua wakazi 9 na kuharibu majengo na miundombinu ya mji wa kaskazini mwa Ukraine wa Chernihiv, maafisa wa mji huo walisema.
Kundi la mataifa yanayozalisha mafuta la OPEC+, baada ya kupoteza uanachama wa Angola miongoni mwa wengine katika miaka ya karibuni sasa linalenga kuikaribisha Namibia kujiunga nalo
Idara ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria imesema kuwa tayari imepata karibu dola milioni 27 kufuatia uchunguzi dhidi ya waziri wa serikali aliyesimamishwa kazi, pamoja na maafisa wengine.
Takriban watu 12 waliuawa na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo, baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa eneo hilo, na kiongozi wa shirika la kiraia walisema Jumapili.
Pandisha zaidi