Baada ya kusaini amri za kiutendaji Jumatatu zikitaka Marekani kujiondosha katika TPP na badala yake kuingia katika makubaliano ya nchi kwa nchi ya kibiashara, Trump ameliita ni “jambo kubwa kwa wafanyakazi wa Marekani- kile ambacho tumekifanya.”
Tathmini iliyofanywa na kituo cha televisheni cha Nielsen kimesema watu milioni 30.6 waliotizama kuapishwa kwa Trump kuingia madarakani ambayo imeipita idadi ya watu milioni 20.6 walioangalia kuapishwa kwa Rais wa zamani Barack Obama katika awamu ya pili ya utawala wake 2013.
“Inaonyesha kuna mambo yanayoweza kuhusiana namna fulani na masuala ya usalama wa taifa na mambo ya kipelelezi, ambapo inawezekana rais ameomba kupewa muhtasari au jumuiya ya kipelelezi imependekeza apokee muhtasari huo.”
Mattis alituma ujumbe wa heri kwa majeshi yote ya Marekani dunia nzima, akipongeza kazi wanazofanya kwa kusema “wao ndio macho na walinzi wa taifa hili” akiahidi kufanya juhudi zake zote “kuhakikisha majeshi yetu yako tayari kupambana leo na siku za usoni.”
Wanawake wanathibitisha kuwa kuweza kupata ushauri wa uzazi wa majira na kupata matibabu kinamama kumechangia zaidi ya kitu chochote kile katika kumwezesha mwanamke katika karne hii ya 20 na tunakokwenda katika karne ya 21 pia.
Rais Donald Trump amesema kuwa ataanzisha “dira mpya” kwa taifa la Marekani ambayo itawajali wafanyakazi ambao wametelekezwa kwa sababu ya kufungwa kwa viwanda na uchumi kutetereka.