Mabadilishano makubwa ya wafungwa yanayojumuisha mateka kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vya yemen yameanza leo baada mazungumzo ya kusitisha makubaliano kumalizika na wajumbe kukubaliana kufanyika duru ya pili.
Ndege ya kwanza imeondoka Sanaa , mji unaoshikiliwa na waasi kuelekea mji wa Aden unaodhibitiwa na serikali baada ya ujumbe wa Saudi Arabia kuondoka bila kuwa na makubaliano mapya lakini kukiwa na mpango wa kukutana tena.
Juhudi zote zinakuja mwezi mmoja baada ya maafisa wa ghuba saudia arabia na Iran ambao wanaunga mkono pande zinazopingana katika mzozo wa yemen kukubaliana kurejesha uhusiano , na kusababisha maelewano zaidi katika eneo hilo lenye matatizo.
Leo wafungwa 322 watasafiri kwa kutumia ndege za shirika la msalaba mwekundu kati ya Sanaa na Aden katika siku ya kwanza ya operesheni ambazo zitapelekea wafungwa 887 kuachililiwa.