Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:50
VOA Direct Packages

UN yanunua meli mpya ya kuhamishia mafuta kutoka meli iliyochakaa ya Yemen


Picha ya meli ya mafuta kwenye bandari ya Hodeidah, Yemen

Umoja wa Mataifa Alhamisi umesema kwamba umenunua meli ya mafuta ya kuhamishia zaidi ya mapipa milioni moja kutoka kwenye meli ya mafuta iliyotelekezwa kwenye ufukwe wa Yemen wa bahari ya Sham, operesheni hiyo ikipangwa kuanza mapema mwezi Mei.

Mratibu wa UN kwenye masuala ya kibinadamu nchini Yemen David Gressly amesema kwamba ununuzi wa meli hiyo mpya ni hatua muhimu katika kusuluhisha tatizo la meli hiyo, kwa jina FSO Safer ambayo imekuwa kwenye ufukwe huo kati ya miaka 7 na 8 iliyopita.

Umoja wa Mataifa umeonya kwa miaka kadhaa kwamba FSO yenye umri wa miaka 47 ilikuwa ni hatari kwa usalama iwapo mafuta yake yangeanza kuvuja baharini, au kuchomeka, na kupelekea janga kubwa la kibinadamu na kimazingira.

Janga hilo linaweza kuathiri mataifa yalio karibu na bahari ya Sham na kugharimu takriban dola bilioni 20 kusafisha mafuta hayo kando na kutatiza safari za meli kutoka Bab al Mandab hadi mfereji wa Suez. Meli hiyo imekuwa kwenye bandari hiyo tangu 2015 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG