Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika wamalizika pande zote zikiridhia malengo yaliyofikiwa

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Afrika waliohudhuria Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika, mjini Washington, DC, Marekani.

Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika ulikuwa na mambo mengi ya kuridhisha na makubwa, malengo ya bilioni ya dola, pamoja na habari kwamba rais atalitembela bara hilo.

Rais Joe Biden alirejea kusisitiza nia ya dhati ya utawala wake barani Afrika – na kuwasihi viongozi katika bara hilo kuheshimu nia ya watu wao.

Rais wa Marekani Joe Biden alihitimisha mkutano wa siku tatu wa viongozi wa Afrika kwa kudokeza kwamba huenda akalitembelea bara hilo.

Rais Biden amesema, “kama nilivyowaambia baadhi yenu – mmenikaribisha katika nchi zenu. Nilisema “Muwe makini kwa kile ambacho mnakitaka kwasababu nitafika huko.” Jamaa maskini siku zote utawaona wakijitokeza. Matajiri ni wale ambao hawafiki huko. Maskini wanakuja na kula chakula chenu na kukaa muda mrefu zaidi kuliko ilivyo kawaida. Sawa, ninatazamia kuwaona wengi wenu katika nchi zenu.”

Ni utani kutoka kwa kiongozi wa taifa tajiri sana duniani, ambaye ametumia muda mwingi siku ya Jumatano kujigamba kuhusu mipango ya Marekani kutoa msaada wa takriban dola bilioni 55 kwa bara hilo kwa ajili ya ukosefu wa usalama wa chakula na ukosefu wa usawa na urithi wenye maumivu wa kikoloni.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Afrika waliohudhuria Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika, mjini Washington, DC, Marekani.

Lakini mbali na utani huo, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa aliiambia VOA kuwa ziara ya rais itakuwa na matokeo makubwa.

Balozi Linda Thomas-Greenfield katika Umoja wa Mataifa anasema’ “hii itakuwa fursa nzuri kwa watu wa Afrika – nchi yoyote, kama rais ataamua kufanya ziara kama hiyo – kwa kweli tunaona nia yetu ya dhati ya kuungana nao.”

Hizi ni ishara kubwa na ahadi nyingi tofauti ya diplomasia iliyo kimya kwa kile ambacho kimetokea katika mkutano huu wa viongozi 50 kutoka Afrika, ambao umejumuisha mikutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na viongozi wa Ethiopia na Congo – nchi zote mbili zikiwa zina mizozo –na uthabiti wa mshirika wa Afrika Magharibi Senegal na Angola huko kusini mwa Afrika ambaye ina sekta kubwa sana ya nishati.

Wachambuzi wanasema Marekani inajaribu kufanya kazi na washirika mbali mbali wa kiafrika – bila ya kujali rekodi yao – katika masuala ambayo tunayawezza kuwa katika msingi wa pamoja.

Cameron Hudson mchambuzi wa masuala ya amani, usalama na utawala kwa Afrika katika kituo cha mkakati na masuala ya kimataifa anasema anadhani kwamba Washington inajaribu kubadili uhusiano wake katika bara hilo na siyo kuwafanya kuwa wategemezi kwa kiongozi yeyote au kundi lolote katika nchi hizo, kwasababu tumeona kuwa nchi hizo bado ni tete, na mshirika wa kimkakati huenda ikagubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kesho.”

Biden pia aliwakaribisha viongozi wa Congo, Gabon, Liberia, Madagascar, Nigeria na Sierra Leone kwa mkutano binafsi siku ya Jumatano, ambapo walijadili kuhusu kuna chaguzi zinazotarajiwa kwa kile ambacho White House inasema ni “wakati muhimu sana kwa demokrasia ulimwenguni.”

Hadharani, Biden alithibitisha uungaji mkono wake kwa uwakilishi zaidi wa Waafrika katika G-20 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bila ya kupuuza mapungufu yao.

Rais Biden alisema “kama viongozi, watu wetu wanatutia moyo. Wanatuamsha kwa uwezekano ambao uko ndani ya mamlaka yetu. Kuwa uwezekano mwingi kama tukifanya kazi pamoja. Wanatuambia ukweli unaouma ambao tunatakiwa kuusikiliza. Na mara nyingine inakuwa shida kuusikiliza. Wanatupa changamoto ya kuheshimu thamini tulizojiwekea katika hati zetu nyingi na tuwajibike inavyostahiki kama tulivyopewa dhamana hii kubwa ya uaminifu.”

Ujumbe mahsusi unaangukia katika masikio ambayo hayasikii. Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 89. Sassou Nguesso (79) wa Jamhuri ya Congo, kama ilivyo kwa rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Wengi wa watu hawa – na wanaume wote hawa viongozi wa nchi isipokuwa mmoja – walisaliwa kabla ya nchi zao kujipatia uhuru, kwenye bara hilo ambalo umri wa wastani ni miaka 18 tu.

Watachukua kitu gani kwenda nacho nyumbani. Mbali ya mifuko iliyojaa na kumbukumbu nzuri?