Sylvia Bongo Ondimba Valentin, ambaye ni raia wa Gabon na Ufaransa, na mtoto mmoja wa kiume wa wanandoa hao anashutumiwa na kiongozi wa mapinduzi kutumia njia za hila katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.
Mtoto wao mkubwa, Noureddin Bongo Valentin, tayari amefunguliwa mashtaka ya rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na waliokuwa wajumbe wa baraza la mawaziri na mawaziri wawili wa zamani.
Sylvia Bongo ameshtakiwa na jaji mchunguzi siku ya Alhamisi na kuamriwa kubaki katika kizuizi cha nyumbani, Andre Patrick Roponat alitangaza kwenye vituo vya Televisheni vya serikali.
Pia anakabiliwa na mashtaka mengine ikiwa ni pamoja na kuficha na kughushi, alisema.
Sylvia Bongo amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani katika mji mkuu Libreville tangu mapinduzi ya Agosti 30.
Ametengwa na mume wake na mawakili wake wa Ufaransa wamewasilisha malalamiko mjini Paris dhidi ya kile walichosema "inaonekana ameshikiliwa mateka".
Bongo mwenye umri wa miaka 64, aliitawala nchi hiyo ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2009, alipinduliwa na viongozi wa kijeshi tarehe 30 mwezi Agosti, muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP