Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:54

Zoezi la kuopoa miili ya watu kwenye Meli ya MV Spice Islander lashindikana


Meli iliyozama kati ya Unguja na Pemba ikiwa na zaidi ya abiria 600
Meli iliyozama kati ya Unguja na Pemba ikiwa na zaidi ya abiria 600

kushindikana kwa zoezi hilo kunatokana na hali mbaya ya bahari na kina kilichozama meli hiyo tofauti na uwezo wa wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini.

Zoezi la kuopoa miili ya watu walionasa kwenye mabaki ya Meli ya MV Spice Islander lililokuwa likifanywa kwa pamoja na Wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini na Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa chini limeshindikana

Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa kushindikana kwa zoezi hilo kunatokana na hali mbaya ya bahari na kina kilichozama meli hiyo tofauti na uwezo wa wazamiaji kutoka nchini Afrika ya Kusini.

Inspekta Mhina amesema kuwa uamuzi wa kusitisha zoezi hilo umetangazwa na Kamanda wa Operesheni hiyo kutoka nchini Afrika ya Kusini Bw. Wayne Combrink, ambapo amesema, wazamiaji wake na wale wa nchini Tanzania wameshindwa kuifikia meli hiyo baada ya kubaini kuwa ilikuwa umbali wa kina cha zaidi ya mita 300 chini ya Bahari. Uwezo wa Wazamiaji hao ni kuzamia kina kisichozidi mita 54 tu.

Kwa hiyo kutokana na hali hiyo, Kamanda huyo amesema wameagiza meli maalum ya Sub Marine kutoka Afrika ya Kusini ili kwenda Tanzania kukamilisha zoezi hilo ambalo amesema lisingewezekana kutekelezwa kwa wazamiaji wenye zana za kawaida pasipo kuwepo kwa chombo hicho.

Wazamiaji hao waliwasili Zanzibar usiku wa Septemba 13 wakiwa katika kundi la watu 16 wakiwemo madaktari wanne pamoja na vifaa vya kisasa wakidhani kina kilichozama meli hiyo kingekuwa chini ya mita 54.

XS
SM
MD
LG