Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 07:55

Zoezi la kuhesabu kura laendelea Mali


Walinzi wa usalama wakiwa katika kituo vya kupiga kura Mali

Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Mali baada ya kumalizika uchaguzi siku ya jumapili, uliokumbwa na vurugu.

Rais Ibrahim Boubacar Keita ambaye kipindi chake cha kwanza madarakani kimekabiliwa na hali mbaya kiusalama anakabiliana na washindani 23 katika kinyang'anyiro cha kuwania urais.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kulikuwa na mashambulizi katika vituo vya kupigia kura na maafisa wa tume ya uchaguzi walikabiliwa na vitisho pamoja na kuwa maafisa usalama 30,000 walisambazwa nchini kote.

Wizara ya uongozi wa mipaka imesema kwamba asilimia tatu ya vituo vya kupigia kura havikufunguliwa, moja ya tano ya vituo vya kupigia kura vikikabiliwa na machafuko mabaya.

Jumla ya vituo 4632 vilikumbwa na vurugu zilizofanywa na watu waliokuwa na silaha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG