Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:32

Zito amuomba Magufuli kushughulikia mgogoro wa Zanzibar


Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-WAZALENDO, bwana Zitto Kabwe
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-WAZALENDO, bwana Zitto Kabwe

Nchini Tanzania chama cha ACT-WAZALENDO kimemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kushughulikia mgogoro wa uchaguzi Zanzibar kwa haraka ili usiweze kuleta mpasuko utakaosababisha machafuko ya kisiasa nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hapo Jumatano, Kiongozi Mkuu wa ACT-WAZALENDO, bwana Zitto Zuberi Kabwe alisema hali ya kisiasa Zanzibar kwa sasa si nzuri hivyo na kwamba ni vyema Rais Magufuli angelipa uzito wa kipekee na kulishughulikia suala hilo kwa haraka

ACT-WAZALENDO chama kichanga kilichosimamisha mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni bi. Anna Mghwila kimejivunia mafanikio hayo ambapo kimepata mbunge mmoja ambaye ni bwana Zitto Kabwe mwenyewe lakini pia kimepata madiwani takribani 50 nchi nzima huku ikifanikiwa kuunda baraza la madiwani katika manispaa ya kigoma ujiji kwa kushinda kata 12.

Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25
Uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25Oktoba 28 mwaka huu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar- ZEC bwana Jecha Salim Jecha alitangaza kufuta matokeo yote ya uchaguzi huko Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 kwa madai kadha wa kadha ikiwemo uchaguzi huo kutokuwa huru na haki.

XS
SM
MD
LG