Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 21:23

Zimbabwe yawatia mbaroni wanaofanya magendo ya kubadilisha fedha


Gavana wa benki kuu Zimbabwe John Mushayavanhu akiwasilisha taarifa yeke ya fedha wakati uzinduzi wa wa sarafu ya ZiG huko Harare April 5 2024. Picha na Jekesai NJIKIZANA / AFP.
Gavana wa benki kuu Zimbabwe John Mushayavanhu akiwasilisha taarifa yeke ya fedha wakati uzinduzi wa wa sarafu ya ZiG huko Harare April 5 2024. Picha na Jekesai NJIKIZANA / AFP.

Mamlaka nchini Zimbabwe imechukua hatua ya haraka kuhusiana na kushuka hivi karibuni kwa sarafu ya dhahabu inayoungwa mkono, kwa kuwakamata wanaofanya magendo ya kubadilisha fedha na kufunga akaunti za biashara zinazotuhumiwa kutumia dola za Marekani peke yake.

Jumatatu wamiliki wa biashara Zimbabwe wamezisihi kamati za bunge kuiomba serikali kuacha kuwakamata wanaobadilisha fedha na kufungua akaunti za makampuni yanayodaiwa kukubali fedha za kigeni tu.

“Huu ni mchakato wa kuanzisha mabadiliko ya sera ya fedha,” alisema Sekai Kuvarika, afisa mtendaji mkuu wa Umoja wa Viwanda Zimbabwe. “Kwa hiyo tujipe muda. Ngoja tulipe soko muda. Tuwape watunga sera muda wa kuangalia upya jinsi gani sera hizo zinafanya kazi katika soko letu. Lakini tuna uhakika hatuungi mkono kuwa tunaambatanisha sera zetu na polisi.”

Wiki iliyopita, polisi waliwakamata watu kadhaa ambao walisema walichochea soko la biashara ya magendo ambako sarafu mpya ya Zimbabwe inayoitwa ZiG ilizinduliwa mapema mwezi huu, inabadilishwa kwa takriban ZiG 20 kwa dola moja ya Marekani.

Kiwango rasmi cha serikali cha kubadilisha fedha ni ZiG 13 kwa dola moja.

Serikali imesema kwa sasa, bidhaa kama vile mafuta na ushuru wa uagizaji bidhaa utabaki kulipwa kwa dola.

Bunge limemuita Waziri wa fedha Mthuli Ncube na Gavana wa Benki Kuu ya Zimbabwe John Mushayavanhu kueleza jinsi gani sarafu ya ZiG itafanya kazi, lakini kwa sababu zisizojulikalikana hakuna aliyehudhuria.

Wiki iliyopita Mushayavanhu alitangaza mabadiliko ya sera za benki kuu — akiapa kurudisha imani katika taasisi ambayo imeshindwa kudhibiti sarafu ya taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG