Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:15

Zimbabwe: uchaguzi mkuu kufanyikamwaka huu


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Katiba mpya ilitakiwa iwe imeshaandikwa mwaka mmoja uliopita, lakini kumekuwepo na uchelewesho mkubwa katika utaratibu huo,

Rais wa zimbabwe Robert Mugabe ameadhimisha miaka 88 ya kuzaliwa kwake hivi kwa kufanya mahojiano kadhaa ambapo amesisitiza kuwa ataitisha uchaguzi baadae mwaka huu.

Hata hivyo wachambuzi wanasema huenda akawakaidi viongozi wa kieneo ambao wanasisitiza kwamba katiba mpya, iidhinishwe katika kura ya maoni, kabla ya uchaguzi kufanyika.

Bwana Mugabe ameiambia televisheni ya taifa ya zimbabwe kwamba anataka uchaguzi ufanyike mwaka huu na kwamba atafanya kila awezalo kuhakikisha unafanyika.

lakini kufanya hivi, bwana Mugabe atakuwa anajiondoa katika mkataba wa mwaka 2008 ambao ulipelekea kuundwa kwa serikali ya kushirikiana madaraka nchini kwake. Mkataba huo unaungwa mkono na jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa afrika – Sadc.

Ibbo Mandaza mwandishi na muanzilishi wa taasisi ya sapes, ambayo inafuatilia masuala ya kieneo, anasema kuliko kupata uungaji mkono wa Sadc na umoja wa afrika, bwana Mugabe huenda akafanya maamuzi peke yake ya kuitisha uchaguzi. Anasema ustahimilivu wao kwa kiongozi huyo mwenye umri mkubwa unaanza kuwaishia.

Sadc ilimteua rais wa afrika kusini Jacob Zuma kuwa mshauri wa kipindi cha mpito cha Zimbabwe. Amepata uungaji mkono wa Sadc na au kwa kile kinachoitwa utaratibu wa Zimbabwe ambao unahitaji utekelezaji kamili wa mkataba wa kisiasa wa mwaka 2008, ikiwa ni pamoja na kuandaa katiba mpya ambayo itaidhinishwa na wazimbabwe katika kura ya maoni.

Katiba mpya ilitakiwa iwe imeshaandikwa mwaka mmoja uliopita, lakini kumekuwepo na uchelewesho mkubwa katika utaratibu huo, na rasimu ya katiba hivi sasa inatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi michacheijayo. Mandaza anasema mara hilo litakapofanyika, kuna utaratibu mwingine ambao nao utachukua muda na lazima ufanyike kwa mujibu wa kanuni.

XS
SM
MD
LG