Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:33

Waziri mkuu wa India aanza ziara ya Afrika


Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na Rais wa Mozambique, Filipe Nyusi
Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, na Rais wa Mozambique, Filipe Nyusi

Waziri Mkuu wa India, Naredra Modi, ameanza ziara ya siku tano barani Afrika hii leo, ambayo itampeleka nchini Tanzania na Kenya kati ya mataifa mengine.

Kulingana na ratiba ya kiongozi huyo, leo anaitembelea nchi ya Mozambique, ambako atakutana na rais wa nchi hiyo, Filipe Nyusi, na kutembelea majengo ya bunge

Jarida la 'The Times of India' limeripoti kuwa serikali ya India ilitia saini makubaliano ambayo yatawasilishwa kwa Serikali ya Mozambique kuhusu uzalishaji wa maharagwe na msaada wa kuimarisha kilimo nchini Mozambique.

Ziara hiyo ya Modi ni ya kwanza kufanywa na Waziri Mkuu wa India nchini Mozambique kwa miaka 34.

Baada ya kuzuru Mozambique, Modi pia atazuru Afrika Kusini kabla ya kuelekea Tanzania na hatimaye kuzuru nchini Kenya.

XS
SM
MD
LG