Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 09, 2024 Local time: 01:01

Ziara ya Trump Ufaransa itavipumzisha vyombo vya habari Marekani


Rais Trump na mkewe Melania wakiwasili Ufaransa
Rais Trump na mkewe Melania wakiwasili Ufaransa

Rais Donald Trump wa Marekani amewasili Ufaransa Alhamisi kwa ajili ya sherehe za Siku ya Bastille.

Sherehe hiyo itashuhudia vikosi vya Marekani na Ufaransa vikifanya gwaride la pamoja Ijumaa katika eneo la Paris linalojulikana kama Champs Élysées.

Ziara hiyo ya siku mbili inaweza ikawa kwa namna fulani ni pumuo kwa vyombo vya habari kuendelea kudadisi juu ya madai ya kuwepo uhusiano kati ya kampeni ya Rais Trump na Russia.

Lakini pia anatarajiwa kukabiliwa na maswali ya ziada wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari huko Paris jioni Alhamisi yakihusiana na mkutano wa mtoto wake wa kiume na mwanasheria wa Russia.

Mtoto wake mdogo Trump alituma barua pepe akionyesha anaamini mkutano huo ulikuwa kwa ajili ya kujadili baadhi ya nyaraka ambazo zingeweza kuchafua kampeni ya mgombea wa Demokratik Hillary Clinton.

Kabla ya kufanyika hafla hiyo, Rais wa Marekani atajaribu kutafuta makubaliano juu ya suala la Syria na mapambano dhidi ya ugaidi, katika mahusiano ambayo yametetereka atapokutana na rais kijana mpya, Emmaneul Macron.

Macron alipata umashuhuri kupitia vichwa vya habari katika mkutano wa NATO mwezi mei, wakati kamera zilipoonyesha akipeana mkono na Rais Trump.

Katika tukio hilo Kiongozi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 39, na mwembamba aliushika mkono wa Trump kwa nguvu kwa dakika kadhaa ambapo vyombo vya habari vilielezea kuwa ilikuwa ni mashindano ya kupimana nguvu za mikono.

Rais Trump anania ya kuonyesha kuwa utawala wake unaendelea kufungamana na washirika wa Marekani wa jadiUlaya.

XS
SM
MD
LG