Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:01

Nigeria yakanusha ziara ya Buhari kuwa ya matibabu


Msemaji wa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amesema ziara ya Rais inayoanza Jumatatu si ya matibabu bali ni ya mapumziko.

Femi Adesina, ambaye ni mshauri mwandamizi wa masuala ya habari, amesema Rais Buhari atatumia likizo yake kufanya uchunguzi wa afya yake na hasa kuangalia kama amepata maambukizo katika sikio lake.

Naibu Rais wa Chama cha Utabibu cha Jumuiya ya Madola ammeonyesha kusikitishwa kwake na safari ya rais ya siku kumi jijini London na kusema inaleta picha mbaya kwa wataalamu wa Nigeria na picha nzima ya nchi.

Dk. Osahon Enabulele amesema utalii wa matibabu unaigharimu Nigeria takriban dola za kimarekani bilioni 1 hasa kutoka kwa viongozi wa kisiasa na umma pamoja na wasaidizi wao.

XS
SM
MD
LG