Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 09:50

Zelenskyy atembelea Marekani kufanya mazungumzo na Biden, kuhutubia Bunge la Marekani


Rais Joe Biden (kushoto) na Rais Volodymyr Zelenskyy
Rais Joe Biden (kushoto) na Rais Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anatembelea Marekani Jumatano na atakuwepo  White House na kuhutubia kikao cha pamoja cha bunge  ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya Ukraine tangu Russia ilipoivamia nchi yake mwezi Februari.

Zelensky aliandika katika mtandao wa Twitter Jumatano, kwamba alikuwa njiani kuelekea Marekani “kuimarisha uthabiti na uwezo wa ulinzi wa Ukraine.”

Afisa mwandamizi wa utawala aliwaambia waandishi wa habari kwamba rais Joe Biden alimwalika Zelensky kukutana naye pamoja na timu yake ya usalama wa taifa na baraza lake la mawaziri. Afisa huyo alisema mazungumzo yatajumuisha ‘majadiliano ya kina ya kimkakati kuhusu njia ya kusonga mbele katika uwanja wa vita,’ ni vifaa gani na mafunzo ambayo Marekani na washirika wengine wanaweza kutoa pamoja na misaada ya kuchumi , nishati na kibinadamu.

Zelenskyy amerejea kuisihi Marekani na wengine kuwapatia mfumo wa ulinzi wa anga ambao utaisaidia Ukraine kukabiliana na mashambulizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani, yanayofanywa na vikosi vya rais wa Russia Vladmir Putin ambavyo vimepiga katika miji kote nchini humo na kuharibu miundombinu yake.

Afisa huyo mwandamizi amesema Marekani itatangaza msaada mpya wa kijeshi kwa ajili ya Ukraine ikiwemo makombora ya masafa marefu ya kujilinda yaitwayo- Patriot , mfumo wa hali ya juu zaidi wa ulinzi wa anga kuliko ule ambao Ukraine imeupata hapo awali.

XS
SM
MD
LG