“Hatuhitaji njia zozote mbadala zaidi ya ombi la Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya, hatuhitaji muafaka kama huu,” Zelenskyy aliwaambia waandishi mjini Kyiv wakati wa mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ureno Antonio Costa walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameibua utata kwa Ukraine hapo Mei 9 alipopendekeza kuwa nchi hiyo ingeweza kuchukua “miongo kadhaa” kuwa mwanachama kamili wa EU na badala yake iombe kujiunga na jumuiya ya kisiasa ya Umoja wa Ulaya,” chombo ambacho ni cha nje ya Umoja wa Ulaya.
Ukraine itatambua kuwa itahitajika kufikia viwango vya kina katika uongozi, kupambana na ufisadi na kutekeleza utawala wa sheria kabla ya kukubaliwa kuingia kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Russia iliivamia Ukraine Februari, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuizuia Kyiv kujiunga na EU na NATO.
Lakini Zelenskyy Jumamosi alisisitiza kuwa nchi yake iruhusiwe kuanza na mchakato wa kuwa mwanachama kamili wa EU.