Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 06:49

Zelenskyy asema Russia imeshindwa kupata njia ya 'kutuangamiza na hataweza kupata fursa hiyo'


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (kushoto) na Rais wa Russia Vladimir Putin

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Alhamisi katika hotuba yake ya usiku, miezi tisa hivi  leo  tangu  uvamizi wa Russia, adui ameshindwa kupata njia ya “kutuangamiza, na hataweza kupata fursa hiyo.”

Zelenskyy ameongeza kuwa majeshi ya Ukraine yanaendelea kushikilia “maeneo muhimu” katika pande zote za nchi hiyo.

Amesema kwamba kusonga mbele kwa wa Ukraine kulikuwa kumepangwa katika baadhi ya maeneo ambayo hayajatajwa.

Matukio mabaya ya miezi tisa yamekuja wakati ambapo sehemu kubwa ya Ukraine bado iko katika giza na bila ya usambazaji maji wa kuaminika kutokana na mfululizo wa mashambulizi ya Russia katika miundombinu ya maeneo ya raia yaliyopelekea kukatika kwa umeme nchi nzima Jumatano.

“Kwa pamoja tumeweza kuvumilia miezi tisa ya vita kamili na Russia haijapata njia yoyote ya kutuangamiza, na haitaweza kupata fursa hiyo,” Zelenskyy alisema.

Alisema majeshi ya Russia yalikuwa yanaendelea kuupiga mabomu mji wa Kherson, ambapo majeshi ya uvamizi yaliutelekeza mji huo mapema mwezi huu. Ulikuwa ndiyo mji mkuu pekee ambao waliuteka hadi sasa wakati wa uvamizi kamili.

Zelenskyy alisema “takriban kila saa moja” kuna ripoti zinakuja za mashambulizi mapya ya anga ya Russia mjini humo, na watu kadhaa walikuwa wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa huko siku ya Alhamisi, kulingana na maafisa wa eneo.

“Vitisho kama hivyo vilianza mara baada ya jeshi la Russia lilipolazimishwa kukimbia kutoka mkoa wa Kherson. Hiki ni kisasi cha yule aliyeshindwa,” Zelenskyy alisema. “Wao hawajui namna ya kupigana. Kitu pekee wanaweza kukifanya kwa wakati huu ni ugaidi. Iwe ni vitendo vya ugaidi vya hujuma ya nishati, au makombora au mizinga – hilo pekee ndio Russia imejishusha kufanya chini ya uongozi wake.”

XS
SM
MD
LG