Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:48

Zelenskyy apongeza matengenezo ya mfumo wa umeme


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, Jumapili amepongeza juhudi za kurejesha mifumo ya uzalishaji umeme.

Mifumo hiyo iliharibiwa na mashambulizi ya Russia, lakini ameuonya umma kuwa ni mapema mno kutangaza ushindi katika kurejesha nishati hiyo.

Zelenskyy amesema wafanyakazi wamefanya kazi nzuri kutengeneza uharibifu uiosababishwa na makombora ya Russia, na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani Ijumaa na kwamba watu wengi hawakupaswa kukabiliwa na kukatika sana kwa umeme Jumamosi na Jumapili.

Amesema kwamba ratiba ya umeme itawekwa kwa mara nyingine tena wakati wiki ya kazi ilianza Jumatatu.

Russia ilifanya wimbi la mashambulizi mfululizo katika vituo vya kuzalishia nishati katika miezi ya karibuni, na kuwafanya mamilioni ya watu kukosa taa, hita ama maji katika kipindi hiki cha baridi kali.

XS
SM
MD
LG