Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 10:55

Zelenskyy aiomba jumuiya ya kimataifa kuhudhuria mkutano wa amani wa Uswizi


Rais wa Ukraine Volodymyr akihudhuria ngongamano la 21 la Shangri-La, Singapore. Juni 2, 2024.
Rais wa Ukraine Volodymyr akihudhuria ngongamano la 21 la Shangri-La, Singapore. Juni 2, 2024.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumapili ameiomba jumuiya ya kimataifa kushiriki kwenye kongamano la amani la Juni 15-16, litakalofanyikia Uswizi.

Kwenye hotuba yake wakati wa kikao cha Shangri-La Dialogue, nchini Singapore, Zelenskyy amehimiza umuhimu wa demokrasia katika kudumisha juhudi za Ukraine kwenye vita vyake dhidi ya Russia, ambavyo sasa vimeingia mwaka wa tatu.

“Muda si mrefu, ilionekana kama ulimwengu ulisambaratika, lakini tumegundua kuwa mataifa mengi yana ari na uwezo wa kushirikiana, hasa kwenye suala la usalama wa pamoja,” Zelenskky amewaambia mamia ya maafisa wa serikali za nje pamoja na wajumbe waliohudhuria kikao hicho.

Alieleza namna msaada kutoka mataifa mengine ya dunia ulivyoisaidia Ukraine kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Russia, wakati pia wakijaribu kuwaokoa baadhi ya watoto wa Ukraine waliokuwa wametekwa na Russia. Matamshi ya Zelenskky yamekuja wakati Ukraine ikiendelea kushambuliwa vikali na Russia.

Maafisa wa Ukraine wamesema kuwa mashambulizi ya Russia ya usiku kucha yakihusisha makombora 100 pamoja na droni yamelenga mfumo wa umeme pamoja na kujeruhi watu 19 kote nchini.

Forum

XS
SM
MD
LG