Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:31

Zelenskiy asema jeshi la Ukraine limesababisha hasara kubwa kwa wanajeshi wa Russia huko Donbas


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy

Jeshi la Ukraine linasababisha hasara kubwa sana kwa vikosi vya Russia karibu na mji wa Vuhledar katika mkoa wa mashariki wa Donbas, Rais Volodymyr Zelensky amesema Jumapili.

“Hali ni ngumu sana. Na tunapambana. Tunawaangamiza wavamizi na kuisababishia Russia hasara kubwa isiyo ya kawaida,” Zelensky amesema katika hotuba ya kila usiku kwa njia ya video.

Zelensky alitaja miji kadhaa ya Donbas, ambapo mapigano yamekuwa yakifanyika kwa miezi kadhaa, akisema kadri Russia inavyozidi kupata hasara huko Donbas, Bakhmut, Vuhledar, Marinka, Kreminna, ndivyo tutaweza kumaliza vita hivi kwa ushindi wa Ukraine kwa haraka.”

Zelensky alisisitiza kuhusu hali ya ulinzi katika sekta nyingine baada ya kile alichokielezea kama mkutano “uliopanuliwa”wa uongozi wa kijeshi.

Mambo yalikuwa yamedhibitiwa karibu na bandari ya Black Sea ya Odesa, amesema, na wanajeshi walikuwa wakilinda mkoa wa kati wa Zaporizhzhia, ambao kwa sehemu kubwa unadhibitiwa na vikosi vya Russia.

XS
SM
MD
LG