“Kituo cha magari, maeneo ya makazi, jengo la ghorofa nyingi, na kituo cha usafiri wa umma vilishambuliwa,” Zelenskiy alisema kwenye mtandao wa kutuma ujumbe wa Telegram.
Ameongeza kuwa “Jeshi la Russia linashambulia vikali kwa makombora mji wa Kherson. Kwa mara nyingine, linaua raia bila huruma .”
Russia ilikanusha kuwalenga raia.
Ukraine iliuteka tena mji wa Kherson mwezi Novemba mwaka jana baada ya miezi minane ukiwa chini ya udhibiti wa Russia, na kulazimisha wanajeshi wa Russia kuondoka katika mji mkuu pekee wa mkoa waliouteka tangu kuivamia Ukraine tarehe 24 Februari mwaka jana. Lakini mashambulizi ya makombora ya Russia kwenye mji huo yanaendelea.
Facebook Forum