Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:20

Idara ya kodi Zambia ZRA yafunga gazeti la The Post kwa tuhuma za kutokulipa kodi


Watu wakiandamana kufwatia kufungwa kwa gazeti la The Post mjini Lusaka, Zambia.

Uwamuzi wa idara ya mapato ya Zambia ZRA kufunga gazeti la The Post, ambalo ni gazeti huru, unalenga kuwanyamazisha vyombo vya habari vinavyoonekana kumkosoa rais aliye madarakani Edgar Lungu na chama chake cha Patriotic Front wanapokaribia uchaguzi mkuu hapo Agasti 11.

Idara ya mapato ya Zambia ZRA ilisitisha operesheni za gazeti la The Post mjini Lusaka jumanne usiku na kufunga Ofisi zao. Hili linakuja kufuatia mzozo baina ya gazeti hilo na idara hiyo ya ZRA juu ya tuhuma kuwa inadaiwa kodi.

ZRA pia iliomba The Post mara moja kulipa dola takriban millioni 5, elfu mia 316 za kodi za nyuma linalodaiwa gazeti hilo. Mzozo huo umekuwa ukiendelea tangu mwaka 2014, pale ZRA ilipoipeleka gazeti hilo mahakamani kwa kutokulipa kodi.

Joseph Mwenda, naibu mhariri mwandamizi wa The Post anasema kufungwa kwa gazeti hilo ni mbinu za kisiasa.

Anasema hatua hiyo inafanywa kuhakikisha gazeti hilo halichapishi habari au kufanya kazi kabla ya uchaguzi wa mkuu wa rais, wabunge na mitaa. Bw Mwenda anasema gazeti hilo litaendelea kulipa kodi kwenye akaunti kotini licha ya kuendelea kwa mzozo na ZRA.

Bw Mwenda anasema idara ya ZRa ilikosa kulipatia gazeti hilo notisi ya siku 10 ambayo anasema, ndio mwendendo wa kawaida , ili kuwajulisha kuhusu hatua inayofwatia.

XS
SM
MD
LG