Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 05:20

Zambia yapata idhini  ya  mkopo wa  IMF wa dola  bilioni 1.3

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa inaonekana nje ya jengo la makao makuu.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa inaonekana nje ya jengo la makao makuu.

Zambia imepata idhini  ya  mkopo wa  Shirika la  kimataifa la Fedha wa dola  bilioni1.3, mpango wa mkopo wa miezi 38 siku ya Jumatano, hatua muhimu katika azma ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika  kurekebisha madeni yake na kujenga upya uchumi ulioharibiwa na usimamizi mbovu pamoja na COVID-19.

IMF ilisema katika taarifa yake kuwa mpango mpya wa Upanuzi wa Mikopo utatoa jumla ya ufadhili wa Haki Maalum za kuchukua milioni 978.2 kama dola bilioni 1.3 kwa viwango vya sasa vya kubadilisha fedha sawa na asilimia 100 ya mgao wa Mfuko wa Zambia, au umiliki wa hisa.

Uidhinishaji wa Bodi ya Utendaji ya IMF utafungua utoaji wa mara moja wa takriban dola milioni 185, Mfuko ulisema

Wadai wa Zambia wakiongozwa na China na Ufaransa waliahidi mwishoni mwa Julai kujadili marekebisho ya madeni ya nchi hiyo, hatua ambayo Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva aliikaribisha kama kusafisha njia kwa mpango mpya wa kuwapa fedha.

XS
SM
MD
LG