Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:51

Upinzani walalamikia Tume ya Uchaguzi Zambia


Waandamanaji nchini Zambia.
Waandamanaji nchini Zambia.

Chama cha upinzani cha Forum for Democracy and Development(FDD) nchini Zambia kimeandikia mahakama ya kikatiba barua rasmi ya kupinga kisheria uamuzi wa tume ya uchaguzi wa kusitisha kampeni za kisiasa kwenye miji ya Namwala na Lusaka kufuatia ghasia za kisiasa zilizoshuhudiwa.

Mahakama ya katiba imeruhusiwa kisheria kusikiliza kesi zinazohusiana na uchaguzi nchini Zambia ndani ya kipindi cha siku 7 baada ya malalamishi kuwasilishwa.

Tume ya uchaguzi imesema imeruhusiwa kisheria kusitisha kampeni kwenye miji hiyo miwili kufuatia ghasia zilizofanywa na chama kiku cha upinzani cha United for National Development UPND.

Ghasia katika eneo la Namwala ziliacha mgombea wa ubunge wa chama cha FDD Charity Kabongomana na majeraha yaliopekea kulazwa hospitalini.

XS
SM
MD
LG