Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:32

Michael Sata, Rais mpya wa Zambia


Michael Sata akizungumza na waandishi wa habari wakati huo akiwa mgombea urais katika kituo kimoja cha kupigia kura mjini Lusaka, Zambia
Michael Sata akizungumza na waandishi wa habari wakati huo akiwa mgombea urais katika kituo kimoja cha kupigia kura mjini Lusaka, Zambia

Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini Zambia Michael Sata ameapishwa rasmi kama Rais mpya wa nchi hiyo

Kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini Zambia Michael Sata ameapichwa kama Rais, na kuadhimisha uchaguzi wa pili wa kidemokrasia nchini humo tangu uhuru wake kutoka kwa Uingereza.

Tume ya uchaguzi ilitangaza mapema Ijumaa kwamba kiongozi huyo maarufu mwenye miaka 74 alimshinda mgombea aliyeko madarakani Rupia Banda baada ya kinyang’anyiro kikali cha urais.

Akibubujikwa na machozi kwenye mkutano na waandishi wa habari, Rais Banda alikubali kushindwa akisema kwamba watu wa Zambia wamezungumza na lazima wote tuwasikilize. Aliwasihi wafuasi wake kuacha vitendo vya kulipiza kisasi, akisema hivi sasa sio wakati wa ghasia.

Wafuasi wa bwana Sata waliandamana mitaani kusheherekea baada ya matangazo ya tume ya uchaguzi ambayo yalitolewa usiku kwa saa za huko.

Baada ya upigaji kura wa Jumanne kulikuwa na ripoti za ghasia kote nchini humo zilizoleta mtafaruku kufuatia kuchelewa kwa matokeo ya uchaguzi. Wanachama wengi wa upinzani walisema walikhofu kuchelewa huko kutaruhusu muda kwa tume kupanga matokeo ya kumpendelea bwana Banda.

Wakati huo huo China imetoa uungaji mkono wa tahadhari kwa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Zambia, baada ya kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini humo Michael Sata kumshinda rafiki wa China, Rais Rupia Banda.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China alisema China ni nchi rafiki kwa Zambia na inaheshimu maamuzi ya watu wa Zambia. Alisema China inataka kufanya kazi na serikali mpya ya Zambia kuhamasisha urafiki na kupanua ushirikiano wao.

Msemaji huyo hakusema kama sera za China kwa Zambia zitabadilika. Bwana Sata ni mwanasiasa wa kitaifa ambaye alifanya kampeni dhidi ya sera za mrithi kwa China.

XS
SM
MD
LG