Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 14:04

Zamaleck yakata tiketi ya kuingia robo fainali BAL


Carlos Morais wa Petro De Luanda akiwa na mpira dhidi ya Zamaleck ya Misri katika uwanja wa Dr Hassan Moustafa Sports Hall mjini Cairo.

Timu ya Zamalek ya Misri ilipata ushindi wake wa tatu katika kanda ya  Nile siku ya Ijumaa, kwa kuwalaza Petro de Luanda ya Angola kwa jumla ya pointi 85-72 katika mchezo ambao ulikuwa wa karibu sana hadi kota ya nne.

Timu ya Zamalek ya Misri ilipata ushindi wake wa tatu katika kanda ya Nile siku ya Ijumaa, kwa kuwalaza Petro de Luanda ya Angola kwa jumla ya pointi 85-72 katika mchezo ambao ulikuwa wa karibu sana hadi kota ya nne.

Zamalek walipata uongozi mapema huku Gonçalves wa Petro akimpatia pasi Gakou anayepachika pointi mbili.

Ulinzi mkali wa Petro haukumzuia Sosa wa Zamalek kufika kwenye kikapu na kupachika pointi mbili.

Zikiwa zimesalia chini ya dakika 3 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Mckinney wa Zamalek alimpasia Mahmoud aliyeurukia na kutumbukiza dunk ambayo iliwaamsha mashabiki uwanjani.

Wakiwa chini ya dakika 5 katika kota ya 3, Strawberry Jr wa Misri alimpasia Mckinney ambaye aliiipatia timu yake pointi mbili.

Mckinney anafanya hivyo tena anapachika pointi mbili zaidi na kufikisha pointi 52.

Misri inaongoza kwa pointi 5 wakati Domingos wa Luanda anampasia mpira Joaquim ambaye alikosa pointi lakini Pedro aliingia na kupachika dunk ya pointi mbili.

Sosa alimpasia Mahmoud aliyeirukia na kutumbukiza dunk nyingine kwa Misri na kuwapa uongozi kwa pointi 8.

Chini ya dakika 3 kabla ya mchezo kumalizika, Sosa alimpasia Mckinney ambaye alipitia katikati na kumpasia Kejo ambaye alipachika pointi mbili.

Misri wamejihakikishia tiketi ya kwenda robo fainali na kuchukua ushindi mwingine kwa kuishinda timu ya Angola kwa pointi 13 katika mchezo wa pili wa Ijumaa.

XS
SM
MD
LG